Spika Mstaafu:Kwa kwa kujitoa kwa dhati katika mambo mbali mbali ya kijamii kutawajengea mwonekano wanawake
Shirika lisilo la kiserikali la TGNP Mtandao leo limekutana na kufanya semina kwa
lengo la kuwajengea uwezo Madiwani wanawake .
katika Warsha hiyo mambo kadhaa ya kijinsia yalizungumzwa huku mgeni rasmi
kuhusiana na mada hizo akiwa ni Anna Semamba Makinda ambaye ameshauri madiwani
hao kupambana na kufikia rekodi kubwa za uongozi kama kufikia rekodi ya kuwa
wabunge wakuchaguliwa majimboni.
Alisema kuwa kuingia katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020 maandali hayo anajua
kuwa yameanza kwani muda uliobaki ni mdogo, kwa hiyo kwa mipango ni bora wawe
wameianze mapema.
Spika huyo mstaafu amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Njombe Kusini katika bunge la
kitaifa nchini Tanzania ambapo pia alikuwa Naibu Spika wa Bunge tangu 2006 hadi 2010,
Spika wa Bunge la Tanzania na Mwaka wa 1990 na 1995 alikuwa Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambapo katika warsha hiyo leo alikuwa kivutiwa
kwa madiwani hao wa Dar es Salaam.
"Viti maalum sio vizuri sana kwani nafasi hizo ata kuzuriwa jambo na kunyang'anywa
nafasi hiyo ni rahisi kwani kwa diwani aliyechaguliwa maamuzi lazima yatakuwa ya watu
waliokuchagua,"alisema Mama Makinda.
Alisema kwa sasa wenye malengo mbali mbali katika kushiriki jambo la uongozi
wanasehemu kubwa ya kuonekana kama kujitoa kwa dhati katika mambo mbali mbali ya
kijamii ambapo hali hiyo itachochea mwonekano wao.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Ujenzi wa nguvu za pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Grace Kisetu alisema kuwa wao kama shirika la kutetea haki za wanawake wapo katika mpango kabambe wa kupigania ongezeko la wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya Ujenzi wa nguvu za pamoja wa TGNP Mtandao Bi. Grace Kisetu alisema kuwa wao kama shirika la kutetea haki za wanawake wapo katika mpango kabambe wa kupigania ongezeko la wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi.
Comments