Ikiwa ni
maadhimisho ya wiki ya utoaji elimu juu ya ugonjwa wa shinikizo la macho
ambayo huadhimishwa duniani kote, takwimu za shirika za afya duniani
zinaonesha kwamba Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 1,740,000 wenye
matatizo yakutoona vizuri.
Akiongea na
vyombo vya habari Leo makao makuu ya Wizara ya afya, naibu waziri wa
afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Faustine ndugulile,
amesema kuwa maadhimisho hayo yalianzishwa kwa lengo la kuongeza uelewa
kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa shinikisho la macho ili kuweza kupunguza
idadi ya watu wasio na uwezo wa kuona.
Pia amesema kuwa
katika maadhimisho hayo kauli mbiu ni "okoa uoni wa macho yako" na
kuongeza kuwa kauli hiyo ni sambamba na ujumbe mahususi kwa jamii kwenda
kwenye vituo vya tiba kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa tatizo la
shinikizo la macho na kusisitiza kuwa kila Mwananchi anapaswa kupima
afya ya macho angala Mara moja kwa mwaka.
Aidha
amebainisha kuwa waathiriwa wakubwa ni watu kutoka bara la Afrika
ikiwemo Tanzania na rika linaloathirika zaidi ni watu wenye umri kuanzia
miaka 40 na kuendela, na huanza na dalili ya kutoona mbali na pia
hutokea kwa kuridhishana kifamilia na pia ugonjwa huzidi kadiri umri wa
kuishi unapokuwa mkubwa.
Pia amesema kuwa
kutakuwa na shughuli za elimu ya afya ya macho pamoja na upimaji wa
afya ya macho kwenye hospitali mablimbali hapa nchini kwa wiki nzima
kuanzia tarehe 11-17 machi kwa wale wote watakaojitokeza kwenye kliniki
ya macho hivyo amewahimiza wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili kiweza
kupima afya ya macho.
Pia amesisitiza
kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kuboresha miundombinu
pamoja na kuongeza wataalamu wa afya ya macho, vifaa na tiba ili
kusogeza huduma za uchunguzi na tiba kwa matatizo ya macho ikiwemo
shinikizo la macho karibu zaidi na wananchi ili kupunguza umbali wa
kifuata huduma ya macho na kuongeza kuwa serikali itasimamia na
kuhakikisha hali ya upatikanaji wa dawa za macho katika vituo vya tiba
inazidi kuimarika zaidi.
Mwisho naibu
waziri amewahasa wananchi kujijengea utaratibu wa kifanya mazoezi ya
mwili na kuepuka kula vyakula visivyofaa na vyenye mafuta mengi na
kusema kuwa wasipokuwa na utaratibu huo itapelekea magonjwa
yasiyoambukizwa kuongezeka jambo ambalo litaigharimu serikali kwa
matibabu ya magonjwa hayo yana gharama kubwa za matibabu.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments