Na Jackline victor Dodoma
Katibu wa baraza la taifa la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Manispaa ya Dodoma Enock Andrew amewahimiza Wazazi kuzingatia kuwapima watoto wao na kufahamu afya zao ili kuweza kuwalinda na kuwaweka katika mazingira salama.
Akizungumza mwandishi wa habari hizi amesema kuwa mwitikio wa wazazi hauridhishi kwani wengi wao hawajiamini katika kupima virusi vya ukimwi na kupelekea kushindwa kuwapeleka watoto wao kwenye vituo vya afya ili kutambua afya ya mtoto.
Katika hatua nyingine amesema kuna watoto ambao wanazaliwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi hivyo inakuwa ni rahisi kwa watoto hao kuweza kutambulika mapema.
Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Dorah Mwauko ameongeza kuwa wanawahamisha wazazi kwa kuwapatia elimu ya umuhimu wa upimaji afya za watoto ili kuweza kuwakinga na maambukizi.
Baadhi ya wazazi wamekili kuwa ni kweli kuna wazazi wamekuwa wakiwalea watoto wao pasipo kujua afya zao na kupelekea kutokuwa na mazoea ya kwenda kupima afya zao wanapokuwa watu wazima.
Comments