Hivi hali hii ulipata kuisoma sawa sawa juzi Real Madrid, na Paris Saint-Germain zote zimeonyesha nia ya kumtaka Salah
Liverpool inakabiliwa na wakati mgumu wa kukataa kitita cha pauni milioni 200 ili kumzuia mshambuliaji wake Mo Salah asiondoke dirisha lijalo la usajili.
Real Madrid, Barcelona na Paris Saint-Germain zote zimeonyesha nia ya kumtaka nyota huyo wa kimataifa wa Misri.
Uwezo wake wa kuzifumania nyavu- magoli 37 katika mechi 43 kwa klabu na nchi yake – umechokoza matamanio ya vilabu vikubwa barani Ulaya.
Inaaminika vilabu hivyo vipo tayari kuvunja rekodi ya pauni milioni 198 iliyolipwa na PSG wakati walipomsajili Neymar kutoka Barcelona kiangazi kilichopita.
Salah ambaye aliigharimu Liverpool pauni milioni 34 kutoka Roma ya Italia, analinganishwa na Lionel Messi. Magoli yake 28 ya Premier League yanamaanisha kuwa amemzidi Messi kwa magoli matatu
.
Comments