kuelekea kilele cha siku ya maadhimisho ya Usonji wakazi wa Jiji watakiwa kuwatunza watoto wenye tatizi hilo
watoto wenye maatatizo ya usonji
Na Mwandishi wetu Dar es salaam
Katika kuelekea kilele cha siku ya maadhimisho ya Usonji (Autism) duniani wakazi wa jiji la Dar es Salaam wametakiwa kuwatunza na kuwalinda watoto wenye maatatizo ya usonji na kujitokeza kwa wingi katika matembezi maalumu yanayotarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa shule za Almuntazir Mohammad Ladack amesema lengo la maadhimisho hayo ni kuelimisha jamii kuhusu watoto wenye Usonji (autism) na kuondoa dhana ya kuwaona watoto hao kama mzigo
Aidha katika shule ya Almuntazir wamefanyika matembezi kwaajili ya kuwajengea watoto hao wenye mahitaji maalumu ambapo wamewagawia maji
Makamu mkuu wa shule ya wasichana Joan Soka amesema watoto hao wametembea lengo likiwa ni kuelimisha na kuwawezesha kufahamu maana ya usonji pamoja na kuwatia moyo watoto
Kwa upande wake mwalimu wa watoto wenye mahitaji maalumu Eva Wigira amesema watoto kama hawa wapo katika jamii na hivyo wana haki ya kupata elimu na wanauwezo mzuri wa kuweza kujifunza na kufanya mambo mbalimbali
Comments