Hispania imefanya maangamizi kwa Argentina baada ya kuichakaza kwa mabao 6-1 katiba bonge la mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa jijini Madrid.
Ikicheza bila washambuliaji wake nyota kama Linel Messi, Aguero na Di Maria, Argentina ilianza kupokea kipigo dakika ya 12 baada ya Diego Costa kuifungia Hispania bao la kwanza.
Isco akaifungia Hispania bao la pili dakika ya 27 kabla ya Nicolas Otamendi hajaipatia Argentina bao pekee dakika ya 39.
Isco ambaye alitupia wavuni jumla ya magoli matatu, akafunga tena dakika ya 52 huku kiungo Thiago Alcantara akiiandikia Hispania bao la nne dakika ya 53 likifuatiwa na lile la Iago Aspas dakika ya 73.
Dakika moja baadae Isco akakamilisha ‘hat trick’ yake kwa kuifungia Hispania bao la sita.
Comments