Old Trafford hakukaliki, Jose Mourinho amekuwa mkali kama
pilipili kiasi kwamba mapumziko ya mechi za kimataifa imekuwa ni ahueni
kubwa kwa wachezaji wa Manchester United.
Ushindi dhidi ya Brighton katika robo fainali ya FA Cup, haukusaidia
kurejesha tabasamu la Mourinho baada ya moto wa lawama aliouwasha Ijumaa
kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.
Katika mchezo dhidi ya Brighton, Mourinho alimkubali mchezji mmoja tu
– Nemanja Matic, lakini wengine wote alisema walicheza soka bovu.
Kocha huyo wa Kireno ameweka wazi kuwa anataka mshiko mrefu ili kukifumua kikosi chake katika usajili wa majira ya kiangazi.
Wakati Fellaini anategemewa kuondoka bure Old Trafford, wachezaji
kama Luke Shaw, Juan Mata, Herreira na Anthony Martial ni miongoni mwa
wachezaji wanahusishwa na panga la Mourinho.
Comments