Jurgen Klopp amepuuzia uvumi kuwa atavunja rekodi ya kuwa kocha
wa muda mrefu zaidi katika Premier League, rekodi inayoshikiliwa na
Arsene Wenger wa Arsenal.
Kocha huyo wa Liverpool amesema miaka 20 ijayo atakuwa na umri wa
miaka 70 na amependa kuwahikikishia mashabiki wa Liverpool hatakuwepo
hapo katika umri huo.
Klopp alisaini mkataba wa miaka sita Liverpool mwaka 2016 ambao
utaisha 2022 lakini haamini kuwa ana nafasi ya kufikia rekodi za Arsene
Wenger na Sir Alex Ferguson kocha wa zamani wa Manchester United.
Amesema kuna tofauti kubwa sana ya makocha wa zamani ambao walikuwa
kwenye utulivu tofauti na soka la sasa hivi ambapo limejaa shinikizo
kutoka kila kona.
Comments