LIVERPOOL KUBEBWA NA HISTORIA KWA MAN CITY …Roma v Barcelona, Juventus v Real Madrid, Sevilla v Bayern
Manchester City na Liverpool zitaumana kwenye robo fainali ya Champions League.
Vilabu hivyo viwili vya Premier League vilikuwa vya mwisho kuibuliwa
kwenye ‘chungu’ cha kupangia ratiba (draw) ya robo fainali ambapo sasa
vijogoo viwili – Jurgen Klopp na Pep Guardiola vitakutana uso kwa uso
mwezi ujao katika vita ya kusaka tiketi ya nusu fainali.
Mechi ya kwanza itachezwa Anfield April 4 huku City ikitwaa nafasi ya kuwa mwenyeji katika mechi ya marudiano wiki moja baadae.
Timu hizo mbili zimeshakutana mara mbili msimu huu katika Premier League huku kila moja ikifaidi ushindi mara moja.
City iliiangamiza Liverpool nyumbani mwezi Septemba kwa ushindi wa
5-0, lakini kikosi cha Klopp nacho kikaibuka na ushindi wa 4-3 katika
mechi ya marudiani iliyochezwa Anfield mwezi Januari.
Kama historia ina faida yoyote katika soka, basi Liverpool itakuwa
kwenye nafasi nzuri ya kwena mechi ya marudiano ikiwa na matokeo mazuri.
City haijawahi kushinda Anfied tangu Mei 2003 – rekodi ambayo Guardiola atahitaji kuivunja.
Robo fainali nyingine itazikutanisha Sevilla na Bayern Munich, Juventus na Real Madrid, Barcelona na Roma
Ratiba ya robo fainali iko kama hivi:
3 April: Sevilla v Bayern, Juventus v Real Madrid
4 April: Barcelona v Roma, Liverpool v Man. City
Mechi za marudiano:
10 April: Roma v Barcelona, Man. City v Liverpool
11 April: Bayern v Sevilla, Real Madrid v Juventus
Comments