Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Premium Lager, ya Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), inatarajia kucheza mchezo wake wa pili wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Demokrasia Congo hii leo siku ya Jumanne Machi 27, 2018, kwenye uwanja wa Taifa.
Huu ni mchezo muhimu katika tarehe zilizopo kwenye kalenda ya FIFA ambapo kocha msaidizi, Hemed Morocco tayari amesema wanauchukulia kwa uzito mkubwa na nia ni kufanya vizuri.
Katika mwezi huu wa Machi, Taifa Stars ilipanga kucheza mechi mbili za kirafiki, kwanza ikiwa tayari imechezwa nchini Algeria dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Kikosi hicho cha Taifa Stars kitaongozwa na nahodha wake Mbwana Samatta anayecheza katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji.
Mbali na Samatta, wachezaji wengine waliyoitwa kwenye kikosi na kocha Salum Mayanga ni pamoja na Aishi Manula, Ramadhan Kabwili, Mohamed Abdulrahman, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondan, Himid Mao Simon Msuva, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Said Ndemla na Shiza Kichuya.
Wengine ni Hassan Kessy, Erasto Nyoni, Shaban Chilunda, Ibrahim Ajib, Yahaya Zayd, Mohamed Issa, Rashid Mandawa na Faisal Salum.
Comments