Kimahesabu Manchester City inahitaji kushinda mechi tatu kati ya nane ilizobakiza ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, lakini hiyo ni iwapo tu Manchester United itashinda mechi zake zote zilizosalia.
Hata hivyo City inaweza ikatwaa ubingwa mapema zaidi iwapo itaifunga Manchester United April 7.
Pamoja na hayo Manchester City pia italazimika kuifunga Everton Machi 31 kabla ya kukutana na mahasimu wao wa jiji la Manchester.
Kwa kufanya hivyo, City itakuwa imefanikiwa kutwaa ubingwa mechi sita kabla msimu haujafikia ukingoni.
Manchester City inaongoza ligi kwa pointi 81 huku ikifuatiwa na United yenye pointi 65
.
Comments