Jiji la Dar es salaam
eneo la clock Tower jijini Arusha
Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Sipora Liana(picha na mtandao)
Salym Bitchuka
Wakuu wa idara wa
Halmashauri ya Jiji na madiwani wote wa jiji la Dar es Salaam wapo Jijini
Arusha kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika masuala mbali mbali na wenzao wa mkoani humo.
Akiwa safarini
kuelekea Jijini Arusha Mkurugenzi wa
jiji la Dar es Salaam Sipora Liana amesema ziara hiyo ni ya siku mbili ikiwa na
lengola kubadilishana uzoefu katika
masuala ya Utalii,Maegesho pamoja na Usafi wa Jiji.
Sipora Liana amesema
kupitia ziara hiyo wanaimani watajifunza vitu vingi katika eneo la
Utalii kwa kuwa wenzao wa Arusha wanauzoefu wa miaka mingi katika eneo hilo.
Aidha mkurungenzi wa
Jiji amesema katika ziara hiyo wametenga
shilingi milioni thelasini lakini ni kiasi cha shilingi milioni 20 ndizo zitakazotumika.
Comments