Mashabiki sasa wanajiuliza kuwa uenda huu ni msimu wa shetani kwa Arsenal, vipigo vya mfululizo vinazidi kumiminika kwa vijana wa Arsene Wenger.
Brighton & Hove Albion imeichapa Arsenal 2-1 katika mchezo mkali wa Ligi Kuu ya England uliofanyika katika dimba la The American Express Community Stadium.
Lewis Dunk aliitanguliza Brighton & Hove Albion kwa bao la kwanza lililotinga wavuni dakika ya 7 kabla Glenn Murray
Hajatupia la pili dakika ya 26.
Arsenal wakapata bao la dakika ya 43 mfungali akiwa ni Pierre-Emerick Aubameyang.
Hii mechi ya nne mfululizo kwa Arsenal kupoteza katika michuano yote, hatu iliyofanya mabango ya 'Wenger Out' yaendelee kushamiri.
Comments