Wiki ya maji imetajwa kuwa inapaswa kuwa ni wiki ya kutatu kero za wananchi amewataka wadau sekta hiyo ya maji kutokaa ofisini na badala yake kwenda kwa wananchi.
Hayo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokuwaakizungumza na
wenyeviti wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani pamoja na Wafanyakazi wa Dawasa
walioudhuria kwenye uzinduzi wa wiki hiyo kwa mkoa wa Dar es Salaam
katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa jijini.
"Dar es Salaam ni jiji la tatu Afrika kwa ukuwaji hivyo mazingira rafiki yanatakiwa yawezeshe kuwa ukubwa ukubwa wake,"alisema Paul Makonda.
Alisema mifumo ya majitaka bado ni tatizo katika jiji hilo na kuagiza wahusika wafanye kazi ya kujituma zaidi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wenyeviti wa Mkoa
wa Dar es Salaam na Pwani pamoja na Wafanyakazi wa Dawasa ambao
wameudhuria kwenye uzinduzi wa wiki ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam
uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere hapa jijini.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza wakati wa
uzinduzi wa wiki ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam ambapo alisema ni
vyema Dawasco wakaongeza usambazaji wa maji katika mkoa huo hili
kusaidia ukuaji wa maendeleo ya Viwanda hapa nchini.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza wakati
wakati wa uzinduzi wa wiki ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika
leo.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akizungumza na wadau wa maji
waliofika katika uzinduzi wa wiki ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam,
pia alieleza mafanikio ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kipindi cha
Miaka Miwili.
Baadhi wafanyakazi wa Dawasa na DAWASCO waliohudhuria kwenye uzinduzi wa wiki ya maji kwa mkoa wa Dar es Salaam.
Sehemu ya Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa wa mkoa wa Dar es Salaam waliohudhuria uzinduzi wa Wiki ya Maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam
Comments