Msanii wa muziki kutoka nchini Marekani, Rihanna amezidi kufikia mafanikio makubwa katika maisha yake ya kimuziki.
Muimbaji huyo wa Pop ameweka rekodi kupitia Apple Music kwa kufikisha wasikilizaji Billion mbili (2 billion steams), Rihanna amekuwa msanii kwanza wa kike duniani kufikia mafanikio hao.
“When I found out that I was the first female artist to cross 2 billion worldwide streams on Apple Music! God is too lit!!!!,” ameandika Rihanna katika Instagram.
March 9 mwaka huu katika kuhadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake duniani Apple Music ilitoa orodha ya wasanii 20 wa kike waliofanya vizuri katika streams ambapo Rihanna alikuwa namba moja akiwaongoza wasanii kama Taylor Swift, Beyoncé, Ariana Grande, Adele, Sia, Lana Del Rey, Selena Gomez, SZA, Lady Gaga na wengine 10.
Comments