KAMPUNI ya Carrer Times Ltd inayoshighulisha na teknolojia imeandaa Africa Technology Awards yenye lengo la kuleta mapinduzi katika hukuaji wa utandawazi wenye manufaa kwa vijana .
Wazo kubwa walilonalo wame jipambanua kuwa ni kusaka wabunifu katika mambo yanayohusu teknolojia na hasa ya habari na mawasiliano nchini.
Aakizungumza jana Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Carrer Time Ltd Hawa Hongo amesema kuwa watatoa tuzo hiyo baada ya kupata washindi kwenye mambo ya ubunifu na kuanzia kesho wataanza kutoa fomu kwa wanaotaka kushiriki.
Amesema vijana wengi ambao wanao uwezo wa kubuni mambo yanayoweza kusaidia maendeleo ya nchi, hivyo wameamua kuchukua jukumu hilo kwa kutoa tuzo hiyo baada ya kushindanisha kazi za ubunifu ambazo washiriki watazionesha kwao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Carrier Time Ltd, Hawa Hongo akizungumza na wanahabari jana katika Ofisi hizo.
.
" Vijana wengi ambao wapo mtaani na wanao uwezo mkubwa katika kubuni mambo yanayohusu teknolojia ndio hasa walengwa katika suala hili , ambapo tunataka kuwaibua kwa maslahi ya nchi yetu.Tunaka vijana ambao wataoesha uwezo wao halisi katika mambo ya ubunifu,"amesema.
Amesema kumekuwepo na mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakiibua vipaji lakini kwenye mambo ya ubunifu katika mambo yanayohusu teknolojia haifanyiki sana na hivyo wao kupitia kampuni yao wameamua kusaka vijapaji vilivyojificha mtaani.
Kuhusu taratibu za kupata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano hayo, alielezea kutakuwa na utaratibu wa uchukuaji wa fumu zitazo tolewa kwenye ofisi zao zilizopo Mikocheni B , mtaa wa Huruma jijini Dar es Salaam.
Comments