Mahusiano yoyote yale huhitaji mtu mwenye uvumilivu, imara,
mkweli na muwazi lakini hivi vyote vikishindikana basi, mahusiano hayo huingia
doa.
Watu kuwa na wapenzi wawili wawili huenda ikawa
sijambo geni, lakini ni jambo geni pale mwezi wako akilifanya.
Matatizo haya yamekuwepo kwa miaka mingi, lakini
sidhani kama yatakuja kuzoeleka, maana kila mmoja hapa anahitaji upendo wa
dhati na wakwake tuu, usio na kugawana na mtu mwingine.
Vitabu vya dini vinasisitiza upendo ulio mmoja
katika mahusiano yaliyohalalishwa na Mwenyezi Mungu mwenyewe, 'tuliheshimu
hili'.
Katika makala hii inayolenga kukuonyesha dalili
za mwenzi wako kutoka nje ya mahusiano, kwa kiasi kikubwa itakusaidia wewe kuwa
sehemu sahihi.
Dalili 6 zitakazokuonyesha kuwa mpenzi wako anamahusiano nje ya ndoa au urafiki
wenu.
1. Mmekuwa wawazi kwa muda sasa, yani mwenzi wako amekuwa akishea na wewe
mambo mbalimbali ya siku nzima, ghafla anaanza kuchelewa kurudi kutoka kazini,
na akirudi hakuambii alikuwa wapi.
2. Umekuwa ukikaribishwa kumtembelea kazini kwake, lakini siku hizi anatengeneza
sababu nyingi za kukuweka mbali na maeneo ya kazini kwake kabisaa.
3. Siku moja unapanda katika gari ya mkeo au mmeo alafu unataka kufungua
kile kibox kilichopo pale mbele ambacho huwa kinatumika kuhifadhia vitu mbali
mbali, mara unakuta kimefungwa kabisa na mwenzi wako anagoma kukifungua.
4. Ghafla
mkeo/mme anaanza kujifungia bafuni anapokwenda kuoga, na hakuwa anafanya hivyo,
je huenda akawa anatumia muda huo kuwasiliana na mtu mwingine kwa njia ya
maandishi?
5. Mke/mme
wako ana mikutano au mitoko na marafiki na kumbuka kukuhusu sehemu wanayokwenda
inautata, mfano disco, bar usiku alafu hakuambii n.k.
6. Mpenzi wako anageuka kuwa
msiri katika mambo yake, yani anakuficha nywila/passwod ya simu au laptop yake,
tofauti na mwanzoni alikuwa anakuweka wazi.
Hayo na mengine mengi yanaweza kukufanya ukaona
kuwa ni sehemu kubwa ya kuwa mumeo/mkeo anamahusiano na mtu mwingine nje ya
mahusiano yenu.
Angalizo: Dalili zote hizo 6
huenda mpenzi wako akawanazo baadhi tu, kwa mfano kuchelewa kazini, usiri wa
kazini n.k hii aimaanishi tu ni msaliti wa mapenzi, hapana wakati mwingine ziko
sababu za msingi zinazo msababisha yeye kufanya hivyo na sio kuchepuka.
Comments