Mwanafunzi aliyepotea Tanzania apatikana akiwa hajitambui
Mwenyekiti wa
Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika
mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani
Iringa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Inadaiwa kuwa alijikuta
katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na
kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi? ambao
walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo
cha polisi kilichoko karibu.
Mahojiano yake katika kituo cha
Polisi Mafinga eneo alikopatikana yamefanyika na baadaye kupiga simu
kwa ndugu zake. Baada ya kupata taarifa ya kupatikana mwanawe, baba
mzazi Mussa Mitumba ameomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili
kujua nini kilimpata mwanae ili aweze kujua kama jambo jingine
alilowaambia kuhusiana na kutekwa kwake.
- Marekani: Tunasikitishwa na vitendo vya utekaji na ukatili Tanzania
- Tundu Lissu asimama kwa mara ya kwanza
- Siku ya 100: Azory Gwanda yuko wapi?
Alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika
hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu
taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini humo,
Tahliso.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) ulisema baada ya
kuondoka afisi hizo, Bw Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka
kwenda nyumbani Madale.
Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo
alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua na
wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao
wamekuwa wakimpatia vitisho.Source http://www.bbc.com
Comments