Skip to main content

TCRA yatoa onyo kali kwa vyombo vya Radio na TV

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kwa Redio na vituo vya runinga nchini kuhusu kupiga nyimbo za wasanii wa muziki ambazo zinakiuka maadili ya mtanzania na vifungu vya sheria ya ya utangazaji.



Afisa Utangazaji TCRA, Rolf Kibaja

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Machi 1, 2018 jijini Dar es salaam, Afisa Utangazaji TCRA, Rolf Kibaja, amesema sheria na kanuni za huduma ya utangazi zipo na lazima zifuatwe na kama kuna Media itakayokiuka itachukuliwa hatua bila huruma.

Comments