Manchester City leo usiku
itakuwa dimbani katika mchezo wa Premier League, kocha wa timu hiyo Arsene Wenger amesema hana
wasiwasi wa kufukuzwa kazi.
Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal) inakumbana na Manchester City huku ikiwa na
kumbukumbu ya kichapo cha bao 3-0 katika mechi ya fainali ya EFL (Carabao Cup)
iliyopigwa Jumapili iliyopita.
Wenger ambaye yuko katika mwaka wake wa 22 tangu aanze
kuifundisha Arsenal, amesema anashangazwa na mjadala wa yeye kusalia au
kutimuliwa Arsenal.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 akang’’aka katika mkutano
wake na waandishi wa habari: "Bado inanishangaza kwamba natakiwa kujibu
maswali ya aina hii".
"Nimeukataa ulimwengu wote kuhakikisha naheshimu
mikataba yangu," ameongeza.
"Nafasi yangu haininyimi usingizi kwa sasa. Wasiwasi
wangu ni jinsi ya kuhakikisha timu inabaki makini na kuwa tayari kwa mechi dhidi
ya Manchester City."

Comments