Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Na Jemsi Salvatory Dar es salaam
Na Jemsi Salvatory Dar es salaam
Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA umemalizika leo Dar es salaam na wanachama kukubaliana maazimio mbali mbali yanayolenga kutekeleza kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, saratani, magonjwa ya moyo na ya mfumo wa hewa.
Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema makubaliano hayo yamelenga kuimarisha na kuboresha sekta hiyo na afya ya wananchi kwa ujumla.
Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa wamekubaliana pia kuongeza uwajibikaji kwenye afya ya mama na mtoto ili kuepusha vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
Waziri Ummy ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, amesema Suala lingine walilokubaliana ni kutilia mkazo suala la heshima kwa wajawazito kwa sababu mawaziri wameshauri pia Tanzania kukitambua Chuo cha Upasuaji cha Afrika Mashariki, Kati na Kusini.
Comments