Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imetengua
uteuzi wa aliyekuwa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa umoja huo,
Jokate Mwegelo kuanzia leo Jumapili 25/03/2018.
Kamati hiyo iliyokutana kwa dharura mchana wa leo mjini Dodoma
iliongozwa na Mwenyekiti wa umoja huo Ndg. Kheri Denis James imesema
kuwa nafasi ya Jokate itajazwa hapo baadaye.
Jokate aliteuliwa na Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi mnamo
Aprili 25, 2017 kuwa Kaimu Katibu Hamasa na Chipukizi wa jumuiya hiyo.
Comments