Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe magufuli ameeleza ajira 30,000 zitatoka kutokana na ujenzi wa reli ya kisasa.
Rais magufuli amesema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kiwango cha Standard Gauge kutoka Morogoro mpaka Makotopora, Dodoma.
“Ujenzi wa reli hii ya kisasa utatoa ajira, inakadiriwa kuwa jumla ya ajira Elfu 30 za moja kwa moja na nyingine laki sita zisizo za moja kwa moja zitatolewa wakati wa ujenzi wa reli hii,” amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli ameongeza kwa kusema kuwa, anataka Tanzania iwe kama Ulaya.
Comments