Mkurugenzi wa utafiti kutoka kwa watetezi wa Rasilimali wasio na mipaka (WARAMI),Philipo Mwakibinga
wanahabari waliofika kwenye mkuatnohuo(picha na blog hii)
Maaskofu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wametakiwa kujikita katika masuala
mahususi yahusuyo dini ikiwemo kutoa elimu kwa waumini ili kutoleta taharuki
kwa jamii.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa utafiti kutoka kwa watetezi wa Rasilimali wasio na mipaka
(WARAMI),Philipo Mwakibinga wakati akizungumza na wanahabari kufuatia , waraka
mzito wa ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka ambao umetolewa hivi karibuni na Baraza la
Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),
Waraka huo umezungumzia masuala mbalimbali kiroho lakini
pia umetaja changamoto za kufikisha kwa waumini wake.
Mwakibinga amesema kuwa viongozi wa dini wanawajibu wa
kiutumishi katika jamii huku wakilinda dhamira yao ya kuhakikisha umoja wanchi
ya Tanzania unabaki kuwa salama kwa namna yeyote ile.
“Watetezi wa Rasilimali wasio na mipaka (WARAMI),tunashangaa
ni kwa nini waraka huu wa salamu za Pasaka haukujikita zaid katika kuwasisitiza
waumini wake kujikita katika kuabadu,kumnyenyekea Mungu,Kusoma biblia na
Maandiko Mengine ya dini na badala yake wakajikita katika maoni yanayong’ata na
kupuliza”amesema Mwakibinga
Amesema Maaskofu wanajaribu kuwaamnisha kwamba waoni wasafi
na kila wanachozungumza ni sahihi .
Comments