Myanmar limejenga kituo katika vijiji ambavyo watu wa Rohingya wamelazimishwa kuyakimbia makaazi yao.
Wanaharakati
wa shirika hilo wamesema watu walioshuhudia na uchambuzi uliofanywa kupitia
picha za Satellite umeonesha kuwa mwezi Januari wanajeshi wa Burma walikuwa
wakisawazisha ardhi ya vijiji vya wa Rohingya kwa kuponda nyumba na hivi
karibuni wamechoma moto eneo hilo.
Msemaji wa
Amnesty International Tirana Hassan ameelezea hatua zillizochukuliwa katika
jimbo la Rakhine kama ''Jeshi kujinyakulia ardhi''.
Serikali
ya Myanmar bado haijatoa tamko lolote kuhusiana na ripoti hiyo ya Amnesty
International.
Comments