Baada ya ukimya wa zaidi ya miaka miwili bila nyimbo mpya, mwimbaji nyota wa dansi Tarsis Masela anakuja na kitu kipya kitakachokwenda kwa jina la “Juu ya Mapenzi”.
Tarsis ambaye pia kwa muda wote huyo amekuwa hana bendi baada ya kuachana na Akudo Impact, ameimbia Saluti5 kuwa wimbo huo utaachiwa rasmi tarehe 10 mwezi huu.
Katika wimbo huo pia atasikika mkali wa bongo fleva, Dully Skyes ambaye ameshirikishwa ndani ya kigongo hicho cha dakika tatu na nusu.
“Nitaachia audio kwanza halafu muda mfupi baadae itafuata video”, alisema Taris Masela.
Comments