Wanasiasa,wanaharakati,wanahabari,viongozi
wa dini pamoja na mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali
wametakiwa kuanzisha utaratibu wa kuheshimu uhuru wa mahakama ikiwemo
kutokutoa kauli za mashinikizo.
Wito
huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa utafiti wa watetezi wa rasilimali
wasio na mipaka WARAMI,Mr Philipo Mwakibinga wakati akizungumza leo
jijini Dar es salaam kufuatia kauli la za baadhi ya wanasiasa kutaka
kuishinikiza mahakama kutoa maamuzi juu ya kesi zinazowakabili wanachama
wenzao.
Mkurugenzi
Mwakibinga amesema ni lazima watu watambue misingi ya mahakama kuwa ni
kwa ajili ya kutenda haki hivyo ni vyema wakaepuka kuingilia uhuru wa
muhimili huo.
Ameeleza
kuwa vyama vya siasa vinapaswa kufata demokrasia kwenye vyama vyao ili
kuweza kufika maamuzi ambayo wanayahitaji kuyafanya kwenye vyama vyao.
"WARAMI
tunapenda kuwakumbusha watanzania kuwa sheria ni KAA LA MOTO,na
unapovunja sheria ujue kuwa umeamua kushika KAA LA MOTO kwa hiyo lazima
ujiandae kuungua,hivyo tunamkumbusha LEMA kuepukana na maneno ya kusema
kukamatwa kwa viongozi wa chama chake ni mkakati uliopangwa na serikali
kwa ajili ya kuwakomoa"amesema Mwakibinga
"Kila
mtanzania anafahamu kuwa Mbowe na CHADEMA wameitumia mikutano ya
kampeni hasa katika chaguzi ndogo za Siha,na Kinondoni kuwatukana
viongozi wa serikali na kumdhalilisha Rais Magufuli,sasa kwa nini
wahangaike kutaka kujihami kuonyesha kuwa wanaonewa?ameuliza Mwakibinga
Hata
hivyo amewashauri wahariri wa vyombo vya habari wanaotaka matamko
kupitia jukwaa la wahariri TEF kuachana na michezo ya kutumika na
wanasiasa kama ambavyo wamewashauri viongozi wa dini hivi karibuni.
Comments