KIKOSI cha Simba kinaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veteran,
wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji Aprili 4.
Katika mazoezi hayo walimu Pierre Lechante na Masud Djuma, waligawa
wachezaji makundi mawili na kuwafanyisha mazoezi ya kufunga tu.
Kundi la kwanza walikuwa wakipiga krosi ambapo mawinga waliokuwa
wanatumika kwa upande wa kulia na kushoto, Mohammed Hussein 'Tshabalala'
na Asante Kwasi, upande wa kulia Ally Shomari na Mwinyi Kazimoto
walikuwa wakipenya kwa spidi na kupiga krosi ambazo zilionekana
kutendewa haki na Juma Luizio na Nicholas Gyan.
Katika upande wa pili, wachezaji wengine wao walikuwa na zoezi maalumu
ambapo hakuna winga anayepitisha krosi, lakini alisimama Mzamiru katika
upande wa kushoto na kulia alisimama Mohammed Ibrahim huku John Bocco na
Laudit Mavugo wao wakiwa na kazi kubwa ya kufunga.
Comments