Baada ya kuvuka hatua ya 16 bora ya Champions League, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema hajali ni timu gani atakayopangiwa nayo kwenye robo fainali.
Liverpool imesonga mbele baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Porto ya Ureno na kulinda ushindi wake wa 5-0 iliyouvuna katika mchezo wa kwanza.
Klopp akaiambia BT Sport: "Kwa kweli sijali, sina hofu. Mchezo unaokuja? hatuchagui mpinzani, tupo tayari kwa timu yoyote ile. Kuna uwezekano wa timu za England kukutana, lakini hilo halina umuhimu wowote kwetu".
Comments