Ikiwa ni siku chache zimepita tangu China ifanye mabadiliko madogo ya katiba na kupitisha sheria ya kiongozi wao, Xi Jinping kuongoza nchi taifa hilo hadi mwisho wa maisha yake, Hatimaye Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa milele ndani ya chama hicho.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, Zimesema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Bwana Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.
Maamuzi hayo ya chama cha CNDD/FDD kumfanya Rais Nkurunzinza kuwa Kiongozi Mkuu wa Kudumu yanajiri wakati Burundi inajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu marekebisho ya Katiba baadae mwezi Mei. Ambapo endapo katiba hiyo ikapitishwa itamuwezesha Rais Nkurunzinza kuweza kuwania Urais mpaka mwaka wa 2034.
Comments