Kocha Arsene Wenger wa Arsenal aliweka wazi kuwa haombei
kukutana na Atletico Madrid ya Hispania katika robo fainali ya Europa
League. Dua lake limejibu.
CSKA Moscow ya Urusi ndiyo watakaokuwa wapinzani wa Arsenal kwenye
robo fainali hiyo huku Atletico Madrid wakipangiwa Sporting Lisbon ya
Ureno.
Arsenal itakuwa timu ya kwanza ya England kukutana na timu ya Urusi katika michuano hiyo tangu ilipoanzishwa.
Kimbembe cha kusafiri kwa maili 36oo kitawakumba vijana wa Wenger kuelekea mechi ya marudiano itakayopigwa Moscow April 12.
Ratiba ya robo fainali ya Europa League iko kama hivi:
RB Leipzig vs Marseille
Arsenal vs CSKA Moscow
Atletico Madrid vs Sporting Lisbon
Lazio vs Salzburg
Mechi za kwanza zitapigwa April 5 na zile za marudiano itakuwa April 12.
Comments