Wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI, Phillipo Mwakibinga amekitaka chama hicho kutoharibu vyombo vya kiusalama na utoaji haki kwa kuvituhumu ili kuficha udhaifu wao wa kuimarisha chama.
“Tulilokusudia kuwaeleza ni hili la namna viongozi wa chadema kupitia mkutano wao wa jana na wanahabari walivyodhamiria kuingilia uhuru wa mahakama kwa kuanza kushinikiza maamuzi ya mahakama,” amesema na kuongeza.
“Wanatakiwa kujua mahakama ni chombo cha haki walitengeneza mazingira ya kuonyesha kuwa viongozi wao hawatendewi haki kama watapata dhamana leo, ilhali wakijua hilo limelenga kuishawishi, kuishinikiza na kuilazimisha mahakama ifanye watakavyo.”
“Chadema waache kuharibu sifa ya vyombo vya usalama hasa idara nyeti ya usalama wa taifa kwa kuwasingizia mambo ya ajabu ajabu kwa ajili ya kuficha udhaifu wao wa kuimarisha chama. Kila mtu makini mwenye akili timamu anafahamu kuwa mwanafunzi Akwilina alifariki baada ya Mbowe kuhamasisha maandamano ambayo hayakuwa na tija yoyote, sasa kitu gani kinawafanya waweweseke kuvuna matunda yao,” amesema Mwakibinga .
Comments