Naodha wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya
Genk,Ubeligiji amesema kuna haja chipukizi wanaocheza ligi ya VPL,
kuangalia soka la nje,ili kupata uzoefu wa kulisaidia taifa.
Samatta anasema mchezaji anayecheza nje,anakuwa amejifunza vitu tofauti
vinavyokuwa vinaibeba Taifa Stars,inapokuwa na majukumu ya kimataifa.
"Taifa Stars, inapendeza iwe na wachezaji zaidi ya sita ambao wanacheza
nje ya nchi,wanakuwa wana mbinu mbalimbali za kuhakikisha hatua
zinapatikana kama ilivyo kwa mataifa mengine,"anasema
Pia amezungumzia umuhimu wa mashabiki kwamba wanapokuwa wanajitokeza kwa
wingi na kuwashangilia,inawapa hamasa ya kujua wanahitaji kuongeza
bidii, ili kupata matokeo.
"Binafsi najua mashabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani,wanaposhangilia
inatupa hamasa wachezaji kujua tunahitaji kupambana kwa watu ambao wapo
nyuma yetu,"anasema.
Comments