Klabu ya Simba ambayo iliondoka jana usiku nchini Tanzania kuelekea
Misri kwa ajili ya mechi ya marudiano na klabu ya Al-Masry kwenye mchezo
wa kombe la Shirikisho, Klabu hiyo imewasili salama nchini humo.
imba SC wametua mjini Port Said nchini Misri wakipitia Addis Ababa
nchini Ethiopia, ambapo wakiwa huko wamekutana na balozi wa Tanzania
nchini humo, Meja General Issa Suleiman Nassor na kupewa baraka zote.
Simba na Al-Masry walitoka sare ya goli 2-2 kwenye mchezo wa kwanza
ambao ulipigwa hapa Tanzania na watahitaji ushindi kwa namna yoyote au
sare ya kuanzia goli 3 ili waweze kusonga mbele.
Comments