WASANII wa muziki wa Bongoflava nchini wameanza kurekodi nyimbo zao
kupitia ujio wa Studio mpya ya Pili Pili Entertainment ambayo awali
ilikuwa ikijihusisha na wasanii wa filamu nchini.
Hali hiyo ya wasanii hao kuanza kuingiza sauti zao kupitia studio hiyo,
imekuja, kuanzia mapema mwezi huu kufuatia kampuni hiyo yenye umaarufu
katika tasnia ya filamu nchini kufungua studio itakayo jishugulisha na
kurekodi muziki .
Kwa mujibu wa meneja wa meneja wa studio hiyo PRosper kiri
alisema kuwa kampuni hiyo inarudi kwa nguvu zaidi baada ya awali
kuwasimamia wasanii nyota Fesail Ismail and baby madaha.
Alisema kwa malengo makubwa wanakuja kusimamia vipaji sahihi vya
muziki kwani, mara baada ya wasanii watakao weza kufnya kazi
nao watakuwa wameweza kuwa sehemu ya ajira kupitia muziki.
"Tayari tumeanza kurekodi kazi za muziki ambapo hadi sasa
wasanii watano wameweza kurekodi chini ya kampuni hii,"alisema
Prosper.
PRosper alisema baada ya kufanya kazi na wasanii kama Baby Madah na
Feisal Ismail waliotokea kwenye Bongo star Seach na makamuzi
yao kuonekana chini ya Pili Pili Entertainment kwa kwa kusimamiwa
kutengeneza albamu kupitia studio zingine wakati huo.
Alisema hivyo wameanza kwa kusajili majina ya wasanii watano
ambapo muendelezo wa siku za usoni utawa utawapa maisha mazuri
wasanii walio chini yao kwani muziki unaendelea kuwa biashara
kubwa duniani.
Prosper ambaye ni msanii wa filamu meneja katika kitengo hicho
amefikia hadhi hiyo ya kuwa meneja kwa kukaa ndani ya Kampuni
ya Pili Pili kwa muda mrefu huku akiwa amefanya vema kwa kazi
za filamu kama Days Of Night,filamu ya dhamira tamthilia ya
Talaka .
Studio hiyo mpya ni sehemu ya kampuni ya ndani ya nyumba ya
pili Pili Sinza jijini hapa, na ipochini ya maprodyuza mahiri
kama Gerry Beats,Sammily(Dr Dre).
Comments