Aliyekua Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amevunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu aondolewe Madarakani, amesema kuwa amekua muhanga wa mapinduzi ya kijeshi.
Akiwa katika nyumba yake ya kifahari mjini Harare Mugabe amekemea mbinu zilizotumika kumuondoa madarakani.
Amesema alikua tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Emerson mnangagwa na angehakikisha mabadiliko ya madaraka ya uhalali na si yale ya kulazimishwa.
Mugabe amesema kuwa Yuko tayari kwa ajili ya Mazugumzo na Mnangagwa ili kulinda katiba yao.
Hakuna uhakika kama rais huyo wa zamani mwenye Umri wa miaka 94 Anataka kurudi madarakani ama la, lakini ni wazi kuwa anadhani amesalitiwa na rais wa sasa Emerson Mnangagwa.
Amesema kuwa hakudhani kama angepoteza imani yake kwa Mnangagwa kwani yeye ndie alimsaidia kuingia serikalini.
''siamini kama yeye Mnangagwa angeweza kuniondoa madaraki , nimemuingiza serikalini, nimemsaidia alipokua jela anataka kunyongwa, sikuwaza kabisa kama siku moja yeye ndio atakua mtu wa kunitoa madarakani''
Aidha Mugabe ameogeza kuwa madaraka ya sasa yameingia kwa njia zisizo halali.
''Lazima tufute aibu hii, ambayo tumejiletea wenyewe, hatuistahili, hatuistahili, hatuistahili , tafadhali hatuistahili kabisa.Tunatakiwa kuwa nchi inayoheshimu katiba, ndio tunaweza kuwa na mapungufu hapa na pale lakini bado lazima tuheshimu sheria.''
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, baadhi ya wazimbabwe wanashangazwa na mkongwe huyo wa miaka 94, na wengine wanaamini kuwa amepoteza uhalisia kabisa baada ya kuongoza kwa miaka 38 , wakati wake sasa umekwisha.Source BBC.
Comments