MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya ccm ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 hadi 2017 akiwasilisha taarifa hiyo Sophia Mjema alisema katika uchaguzi ujao wa mwaka 2020 Chama cha mapinduzi itachukua dola.
Mjema alisema katika wilaya ya Ilala chama cha mapinduzi itashinda chaguzi za Kata na kuzoa viti vya ubunge vyote na kuendelea kushika dola .
"Wilaya ya Ilala kwa sasa INA madiwani 49 katika baraza la madiwani kati ya madiwani 49, Madiwani 17 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA , madiwani 21 wa Chama cha Mapinduzi CCM na madiwani saba wa Chama cha Wananchi CUF na Wabunge watatu " alisema Mjema.
Mjema amesema hali ya kisiasa kwa sasa Wilaya ya Ilala safi katika utekelezaji wa Ilani .
Akielezea muundo wa Utawala wilaya hiyo INA tarafa TATU kata 36 na mitaa 159, tarafa ya KARIAKOO ina kata kata 13 mitaa 23, Tarafa ya Ilala kata 14 mitaa 75 na tarafa ya Ukonga Kata 9 mitaa 61 majimbo ya uchaguzi matatu
Ilala kata 10, Ukonga Kata 13 na Jimbo la SEGEREA kata 13.
Amesema katika Wilaya hiyo kwa mujibu wa sensa ya makazi iliyofanyika Kitaifa 2012 wilaya INA wakazi jumla 1,220 , 611 wakiwemo Wanaume 595,928 na WANAWAKE 624,683 kufuatia ongezeko la Watu la asilimia 5.6 kwa mwaka kwa sasa 2016 idadi ya wakazi inakadiriwa kufikia 1, 515,359
Wanaume 739,830 na WANAWAKE 775,529.
Akizungumzia shughuli za kiuchumi kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Idara ya Takwimu ya Taifa (NBS) inakadiriwa kuwa asilimia 43,97 ya wakazi wa Ilala wameajiliwa katika sekta binafsi na sekta ya Umma na asilimia 56 .03 wamejiajili wenyewe na katika sekta binafsi wanajishughulisha na shughuli ndogondogo uvuvi ,kilimo na ufugaji wastani wa pato la mkazi wa wilaya hiyo ni sh. 1,73 4,842 kwa mwaka.
" Utekelezaji wa mpango wa Ilani sekta ya fedha kwa mwaka wa fedha 2017 hadi 2018 mpango wa Ilani umelenga kuendelea kuboresha takwimu za Walipa kodi wetu kutoka katika chanzo cha Mapato kuendelea kununua vitendea kazi hususani magari ya kufuatilia mapato na vifaa vya Kielektroniki vya kupokelea mapato, Kukusanya jumla ya sh, 59 , 991 kutoka vyanzo vya ndani" alisema .
Mjema akielezea sekta ya huduma za jamii katika kutekeleza Ilani ya mwaka 2017 hadi 2018 mpango umelenga kuandikisha watoto 7,460,wa Shule za awali na watoto 19, 705 darasa la kwanza katika shule za msingi na kununua madawati 2000, ujenzi wa vyumba vya madarasa 50,matundu ya vyoo 145 na ujenzi wa OFISI nane za Walimu .
Wakati huohuo Sophia Mjema amemtaka Mkurugenzi wa Ilala kuwachukulia hatua Wenyeviti wa Mtaa wanaotoza sh.2000, hadi 5000 kwa wananchi wakienda kuomba Barua ya utamburisho bila kujali chama anachotoka iwe CCM au chama cha upinzani kwani utawala bora hauruhusu kuwahudumia wananchi kwa malipo.
Amewagiza Wajumbe wa Halmashauri kuu kuchukua rekodi ya Wenyeviti wa Mtaa wenye tabia hiyo.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments