Skip to main content

Posts

Showing posts from March, 2018

Argentina ilikichezea kwa mabao 6-1 katiba bonge la mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa jijini Madrid

Hispania imefanya maangamizi kwa Argentina baada ya kuichakaza kwa mabao 6-1 katiba bonge la mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa jijini Madrid. Ikicheza bila washambuliaji wake nyota kama Linel Messi, Aguero na Di Maria, Argentina ilianza kupokea kipigo dakika ya 12 baada ya Diego Costa kuifungia Hispania bao la kwanza. Isco akaifungia Hispania bao la pili dakika ya 27 kabla ya Nicolas Otamendi hajaipatia Argentina bao pekee dakika ya 39. Isco ambaye alitupia wavuni jumla ya magoli matatu, akafunga tena dakika ya 52 huku kiungo Thiago Alcantara akiiandikia Hispania bao la nne dakika ya 53 likifuatiwa na lile la Iago Aspas dakika ya 73. Dakika moja baadae Isco akakamilisha ‘hat trick’ yake kwa kuifungia Hispania bao la sita.

Wekundu wa Msimbazi waendelea kujiweka fiti Uwanja wa Boko Veteran

 KIKOSI cha Simba kinaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veteran, wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji Aprili 4. Katika mazoezi hayo walimu Pierre Lechante na Masud Djuma, waligawa wachezaji makundi mawili na kuwafanyisha mazoezi ya kufunga tu. Kundi la kwanza walikuwa wakipiga krosi ambapo mawinga waliokuwa wanatumika kwa upande wa kulia na kushoto, Mohammed Hussein 'Tshabalala' na Asante Kwasi, upande wa kulia Ally Shomari na Mwinyi Kazimoto walikuwa wakipenya kwa spidi na kupiga krosi ambazo zilionekana kutendewa haki na Juma Luizio na Nicholas Gyan. Katika upande wa pili, wachezaji wengine wao walikuwa na zoezi maalumu ambapo hakuna winga anayepitisha krosi, lakini alisimama Mzamiru katika upande wa kushoto na kulia alisimama Mohammed Ibrahim huku John Bocco na Laudit Mavugo wao wakiwa na kazi kubwa ya kufunga.

Soma Twaweza wanavyoendelea kujipambanua zaidi

ambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Email   Mshirikishe mwenzako Haki miliki ya picha TWAWEZA Image caption Wananchi wangependa kuwa huru kukosoa watawala iwapo hawataridhika na maamuzi ya Serikali Idadi kubwa ya wananchi (60%), nchini Tanzania wanasema hawako huru kukosoa kauli zinazotolewa na Rais wakati asilimia 54 wanasema hivyo kuhusu kauli zinazotolewa na Makamu wa Rais na asilimia 51 Waziri Mkuu. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la utafiti lisilo la serikali, Twaweza. Wananchi wanajisikia huru zaidi kuwakosoa wabunge wao kuliko wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Kwa mujibu wa shirika la Twaweza, hali hii inaweza kuwa ni kwa sababu wananchi wanawachagua wabunge kuwa wawakilishi wao na hivyo wanaona kuwa mbunge anajukumu la kusikiliza mahitaji na vipaumbele vyao na kuvifanyia kazi ipasavyo. Wananchi wanaunga mkono kwa kiasi kikubwa uhuru ...

Changamoto mbalimbali kwa wakunga zaelezwa

Mkurugezi wa huduma za uuguzi na wakunga kutoka Wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsi,wazee na watoto  Gustav Moyo   Katibu mkuu wa Chama cha Wakunga Tanzania-TAMA, Dkt. Sebalida Leshabari baadhi ya wadau wakiwemo waandishi wa habari waliohudhuria kwenye hafla hiyo Na Hellena Matale Dar es salaam Imeelezwa    kuwa wauguzi na wakunga hapa nchini wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupatwa na matatizo ya kuumwa mgongo hali inayowafanya washindwe  kufanya kazi kwa muda mrefu kama inavyotakiwa. Hayo yamesemwa na Mkurugezi wa huduma za uuguzi na wakunga kutoka wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsi,wazee na watoto Gustav Moyo  wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa linalojishuhulisha na idadi ya watu (UNFPA). Amesema kuwa hapa nchini bado  kuna uhaba wa wakunga na waguzi  hali ambayo imekuwa ikichangia  mkunga ...

Soma Naodha wa Taifa Stars anavyofunguka

Naodha wa Tanzania anayekipiga  katika klabu ya Genk,Ubeligiji amesema kuna haja chipukizi wanaocheza ligi ya VPL, kuangalia soka la nje,ili kupata uzoefu wa kulisaidia taifa. Samatta anasema mchezaji anayecheza nje,anakuwa amejifunza vitu tofauti vinavyokuwa vinaibeba Taifa Stars,inapokuwa na majukumu ya kimataifa. "Taifa Stars, inapendeza iwe na wachezaji zaidi ya sita ambao wanacheza nje ya nchi,wanakuwa wana mbinu mbalimbali za kuhakikisha hatua zinapatikana kama ilivyo kwa mataifa mengine,"anasema Pia amezungumzia umuhimu wa mashabiki kwamba wanapokuwa wanajitokeza kwa wingi na kuwashangilia,inawapa hamasa ya kujua wanahitaji kuongeza bidii, ili kupata matokeo. "Binafsi najua mashabiki ni mchezaji wa 12 uwanjani,wanaposhangilia inatupa hamasa wachezaji kujua tunahitaji kupambana kwa watu ambao wapo nyuma yetu,"anasema.

Chanzo kingine kilicho ripoti habari ya WARAMI jana

Watetezi wa Rasilimali za Taifa Wasio na Mipaka-WARAMI wamekionya chama cha Chadema kutoingilia uhuru wa mahakama kwa kutoa matamko ya kuipa mashinikizo katika kutekeleza majukumu yake. Wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI, Phillipo Mwakibinga amekitaka chama hicho kutoharibu vyombo vya kiusalama na utoaji haki kwa kuvituhumu ili kuficha udhaifu wao wa kuimarisha chama. “Tulilokusudia kuwaeleza ni hili la namna viongozi wa chadema kupitia mkutano wao wa jana na wanahabari walivyodhamiria kuingilia uhuru wa mahakama kwa kuanza kushinikiza maamuzi ya mahakama,” amesema na kuongeza. “Wanatakiwa kujua mahakama ni chombo cha haki walitengeneza mazingira ya kuonyesha kuwa viongozi wao hawatendewi haki kama watapata dhamana leo, ilhali wakijua hilo limelenga kuishawishi, kuishinikiza na kuilazimisha mahakama ifanye watakavyo.” “Chadema waache kuharibu sifa ya ...

Sikia anavyozungumza nyota wa soka Bongo Kiemba

  Kiungo  wa  zamani  wa Simba Amri Kiemba  amefunguka kuwa, idadi kubwa  ya wachezaji  wa  Tanzania inawache wenye vipaji lakini  lakini nchi kama Afrika kusini inatuzidi kuwa na vipaji vilivyo pata mafunzo toka vikiwa vichanga huo ndio utofauti wetu na nyota wenye vipaji barani Afrika. Kiemba

Mwansasu FAT ilimkera !!

 Cheki  Mwansasu anavyo jumuika kwenye anga za bata hivi sasa akiwa na mwonekano huo wa mwisho kutoka kulia. Pichani kulia ni  John Mwansasu , ambaye alikuwa beki wa  Yanga  na timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars.Lakini pia nyota huyo katika kipindi hicho cha miaka ya nyuma ,  ngome ya  Yanga  iliyokuwa ikiongozwa na  beki huyo  ilikaa vyema na kuzuia hatari zote zilizokuwa zikielekezwa langoni mwao. Anasema hali ya mbaya ya uongozi wa FAT wakati huo ndio iliyomfanya kuachana na soka .  kweli huyo ni mmoja wa mabeki tishio nyakati hizo.

WARAMI:Wasisi tiza kuheshimu uhuru wa mahakama

Wanasiasa,wanaharakati,wanahabari,viongozi wa dini pamoja na mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali wametakiwa kuanzisha utaratibu wa kuheshimu uhuru wa mahakama ikiwemo kutokutoa kauli za mashinikizo. Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa utafiti wa watetezi wa rasilimali wasio na mipaka WARAMI,Mr Philipo Mwakibinga wakati akizungumza leo jijini Dar es salaam kufuatia kauli la za baadhi ya wanasiasa kutaka kuishinikiza mahakama kutoa maamuzi juu ya kesi zinazowakabili wanachama wenzao. Mkurugenzi Mwakibinga amesema ni lazima watu watambue misingi ya mahakama kuwa ni kwa ajili ya kutenda haki hivyo ni vyema wakaepuka kuingilia uhuru wa muhimili huo. Ameeleza kuwa vyama vya siasa vinapaswa kufata demokrasia kwenye vyama vyao ili kuweza kufika maamuzi ambayo wanayahitaji kuyafanya kwenye vyama vyao. "WARAMI tunapenda kuwakumbusha watanzania kuwa sheria ni KAA LA MOTO,na unapovunja sheria ujue kuwa umeamua kushika KAA LA MOTO kwa hiyo la...

Chadema :Viongozi sita wa upinzani waachiliwa kwa dhamana

Haki miliki ya picha CHADEMA MEDIA Image caption Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema, Freeman Mbowe katika mahakama ya Kisutu Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imewaachia huru kwa dhamana viongozi sita wa Chadema pasipo viongozi hao kuwepo mahakamani Hata hivyo watatakiwa kuripoti kituo cha polisi Kila siku ya Alhamisi. Tanzania: Viongozi sita wa upinzani waachiliwa kwa dhamana Miguna asafirishwa tena kutoka Kenya Akitoa uamuzi wake, Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri amewataka washtakiwa hao kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kusaini kwa maandishi dhamana ya Sh milioni 20."Kila mshtakiwa atasaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 20, wadhamini pia watasaini kiwango hicho, washtakiwa wakiwa nje kwa dhamana wanatakiwa kuripoti polisi mara moja kwa wiki, ambayo ni kila siku ya Alhamisi," amesema Hakimu Mashauri. Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa ni miongoni mwa wanachana na viongozi wa juu wa Chadema waliofika kufuatilia mwenendo wa kesi inayowakabili Mbow...

Carrer Times Ltd yaandaa Africa Technology Awards

KAMPUNI ya Carrer Times Ltd inayoshighulisha na teknolojia imeandaa Africa Technology Awards yenye lengo la  kuleta mapinduzi  katika hukuaji wa utandawazi  wenye manufaa kwa vijana . Wazo kubwa walilonalo  wame jipambanua kuwa ni  kusaka wabunifu katika mambo yanayohusu teknolojia na hasa ya habari na mawasiliano nchini. Aakizungumza jana  Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Carrer Time Ltd Hawa Hongo amesema kuwa watatoa tuzo hiyo baada ya kupata washindi kwenye mambo ya ubunifu na kuanzia kesho wataanza kutoa fomu kwa wanaotaka kushiriki. Amesema vijana wengi ambao wanao uwezo wa kubuni mambo yanayoweza kusaidia maendeleo ya nchi, hivyo wameamua kuchukua jukumu hilo kwa kutoa tuzo hiyo baada ya kushindanisha kazi za ubunifu ambazo washiriki watazionesha kwao. Mkurugenzi wa Kampuni ya Carrier Time Ltd, Hawa Hongo akizungumza na wanahabari jana  katika Ofisi hizo. . " Vijana wengi ambao wapo mtaani na wanao uwezo mkubw...

Ufaransa yaitandika Urusi 3-1

Paul Pogba ameibua matumaini mapya juu ya kiwango chake baada ya kufunga bao la ‘maajabu’ wakati timu yake ya taifa ya Ufaransa ikiitandika Urusi 3-1 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa. Pogba amekuwa na msimu mbaya chini ya kocha Jose Mourinho huko Old Trafford, lakini bao lake tamu la free-kick lililowasili dakika ya nne baada ya mapumziko likaibua hisia kali. Baba wa kiungo huyo wa Manchester United – Fassou Antoine, aliyefariki mwezi Mei mwaka jana, angetimiza miaka 80 Jumanne usiku na ndipo Pogba akatumia mechi hiyo kama kitu maalum kwaajili ya siku ya kuzaliwa baba yake. Baada ya kufunga bao lake akashangilia na kufunua jezi yake ili kuruhusu maandishi aliyoyaandika kwenye fulana yake ya ndani yasomeke. Fulana hiyo iliandikwa ‘Bon Anniversaire, Papa. Allah y Rahmou,’ kwa tafrisi nyepesi yakimaanisha ‘heri ya siku ya kuzaliwa baba, Allah (Mungu) akurehemu’. Kylian Mbappe aliipa Ufaransa bao la kuongoza dakika ya 41 baada ya kazi nzuri ya Pogba na ukingo...

Utoaji Wa Vitambulisho Kwa Wafanyabiashara Wadogo vyazinduliwa na TRA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo imezindua rasmi utoaji wa vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi ikiwa ni pamoja na Wamachinga. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Charles Kichere amesema kuwa, utoaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo unatokana na marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 yaliyofanywa na Bunge la Bajeti la Mwaka wa Fedha 2017/2018 ambapo moja ya marekebisho hayo ni kuwatambua na kuwapatia vitambulisho maalum wafanyabiashara wadogo walio kwenye sekta isiyo rasmi. Baada ya marekebisho ya Bunge la Bajeti la Mwaka wa Fedha 2017/2018, zoezi hili la kuwatambua wafanyabiashara wadogo lilianza kutekelezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) pamoja n...

Yasikie kwa mbali mambo ya Diego Costa

Hispania imefanya maangamizi kwa Argentina baada ya kuichakaza kwa mabao 6-1 katiba bonge la mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa jijini Madrid. Ikicheza bila washambuliaji wake nyota kama Linel Messi, Aguero na Di Maria, Argentina ilianza kupokea kipigo dakika ya 12 baada ya Diego Costa kuifungia Hispania bao la kwanza. Isco akaifungia Hispania bao la pili dakika ya 27 kabla ya Nicolas Otamendi hajaipatia Argentina bao pekee dakika ya 39. Isco ambaye alitupia wavuni jumla ya magoli matatu, akafunga tena dakika ya 52 huku kiungo Thiago Alcantara akiiandikia Hispania bao la nne dakika ya 53 likifuatiwa na lile la Iago Aspas dakika ya 73. Dakika moja baadae Isco akakamilisha ‘hat trick’ yake kwa kuifungia Hispania bao la sita.