2. Kamati
ilibaini kuwa Mkataba wa mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba
ulimalizika Mei 31 mwaka huu. Hivyo kwa taratibu za usajili mchezaji
Kevin Yondani kuanzia Juni 1 mwaka huu alikuwa ni mchezaji huru.
3.
Aidha Kamati ilibaini kuwa Mkataba uliowasilishwa na Klabu ya Simba TFF
ukiwa na maana ya kuongeza mkataba uliokuwepo TFF baina ya mchezaji
Kevin Yondani na Klabu ya Simba uliwasilishwa TFF, Juni 7 mwaka huu
ambapo ni kinyume cha utaratibu wa kuongeza mikataba ya wachezaji
unaozitaka klabu kuwasilisha mikataba ya kuongeza muda wa mikataba ya
wachezaji wao wakati mkataba halisi haujaisha muda wake. Hivyo mkataba
huo kwa jicho la kisheria haupo.
4. Hata kama kamati
ingeuona mkataba huo katika jicho la sheria, bado mkataba huo una
tatizo la kisheria hasa katika tarehe ambazo pande mbili husika
ziliingia makubaliano hayo. Ukiuangalia mkataba huo unabainisha kuwa,
wakati mchezaji Kevin Yondani aliingia makubaliano Desemba 23 mwaka
jana, upande wa pili wa kimkataba ambao ni Klabu ya Simba inaonekana
iliingia makubaliano hayo kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Geofrey
Nyange Kaburu, Desemba 23 mwaka huu.
5. Kisheria utata
huu unaweza kuondolewa na pande husika tu kwa kurekebisha dosari hiyo
kwa maridhiano kuweka saini katika mabadiliko hayo ili kuthibitisha
mabadiliko hayo. Hivyo katika jicho la kisheria mkataba huo hauwezi
kutumika kumzuia mchezaji huyo kwenda katika klabu anayoipenda wakati
akiwa huru. Kutokana na maelezo yote hapo juu, Kamati imeridhia hatua
iliyochukuliwa na Sekretarieti ya TFF ya kumruhusu mchezaji Kevin
Yondani kuichezea timu ya Yanga katika mashindano ya Kombe la Kagame
2012.
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Comments