Serena na Venus wakiwa na vikombe walivyotwaa katika michuano ya wazi ya tennis ya wachezaji wawili wawili ya Wimbledon
Serena na Venus wakipongezana na wapinzani wao baada ya mchezo kumalizika
Serena akirudisha mpira kwa nguvu kwa mpinzani wake wakati wa fainali ya mchezaji mmoja mmoja
Serena akipongezwa na baba yake, Richard William mara baada ya kutwaa taji la mchezaji mmoja mmoja. Kushoto ni dada yake, Venus
Serena akishangilia kwa kulala uwanjani baada ya kushinda taji la tennis la Wimbledon
Serena akinyanyua juu tuzo aliyozawadiwa baada ya kushinda taji la tennis la Wimbledon
Saa
chache baada ya kutwaa taji la michuano ya wazi ya tennis ya Wimbledon
kwa mchezaji mmoja mmoja, Serena Williams alifanikiwa kutwaa taji la
wachezaji wawili wawili kwa kushirikiana na dada yake, Venus Williams.
Katika
mechi hiyo ya fainali iliyokuwa na ushindani mkali, Serena (30) na
Venus (32) waliwabwaga Andrea Hlavackova na Lucie Hradecka wa Jamhuri ya
Czech kwa 7-5, 6-4.
Taji alilotwaa Serena kwa wachezaji
mmoja mmoja baada ya kumbwaga Radwanska lilikuwa la tano katika rekodi
yake na la 14 katika michuano mbalimbali ya mchezo huo.
Safari hii Venus alishindwa kufika mbali katika michuano hiyo baada ya kutolewa raundi ya tano na Elena Vesnia wa Russia.
Venus
na Serena waliwahi kutwaa taji la wachezaji wawili wawili katika
michuano ya Wimbledon kuanzia mwaka 2000, 2002, 2008 na 2009
Comments