CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Kagera kimeisambaratisha ngome ya Waziri wa
Ujenzi, John Magufuli, baada ya kufanikiwa kuwahamisha viongozi na
wanachama 80 wa CCM akiwamo kada maarufu, Dk. Benedictor Lukanima.
|
Vua gamba vaa gwanda ndani ya Chato. |
Viongozi na wanachama hao wa CCM wakiongozwa na Dk. Lukanima,
ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe na mtafiti katika Chuo
Kikuu cha Norte kilichopo nchini Colombia, walitangaza rasmi kuvua
gamba na kuvaa gwanda katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika
juzi kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chato mjini, na kuongozwa na
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Kagera, Alfred Mganyizi Rwagatare.
|
Mwenyekiti wa
CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama
wa chama hicho, Wilfred Lwakatare akimkabidhi kadi ya uanachama wa
CHADEMA Dk. Lukanima |
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jimbo
na wilaya hiyo ya Chato, Wana CCM hao waliohamia CHADEMA walikiponda
vikali chama tawala, kwa madai kwamba serikali yake imeshindwa
kuwasaidia wananchi kuondokana na kero nyingi, ukiwemo umaskini wa
kupindukia unaozidi kuota mizizi hapa nchini.
|
Mwenyekiti wa
CHADEMA wa Mkoa wa Kagera ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama
wa chama hicho, Wilfred Lwakatare akimkabidhi kadi ya uanachama wa
CHADEMA Makonzela Phinias. |
Baadhi ya viongozi wa CCM waliohamia CHADEMA ni pamoja na
Makonzela Phinias ambaye alikuwa mjumbe wa UVCCM na mwakilishi wa
mkutano mkuu wa Vijana Mkoa wa Geita, Masunga Maswanzali, ambaye
alikuwa mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Nyasenga, Kijiji na
Kata ya Ilemela, Josephat Manyenye ambaye amewahi kushika nafasi
mbalimbali za uongozi ndani ya CCM pamoja na Dk. Benedictor Lukanima,
ambaye mwaka 2010 alishika nafasi ya pili katika kura za maoni ndani ya
chama hicho tawala.
|
Makusanyo ya kadi yakiendelea. |
Akihutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kagera
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred
Lwakatare alimrushia kombora zito Waziri Magufuli kwa madai kwamba,
kiongozi huyo ameshindwa kuondoa kero nyingi zinazowakabili wananchi wa
jimbo hilo, ikiwamo ya uhaba wa huduma ya maji, afya, elimu na fursa za
kiuchumi jimboni humo.
|
Kadi zilizorejeshwa. |
Lwakatare alimuita Dk. Magufuli bingwa wa takwimu aliyeshindwa
kuwaletea maendeleo wananchi wake, licha ya kuwa waziri kwa muda mrefu
serikalini. "Magufuli ni bingwa mkubwa wa takwimu. Anaweza kuwaambieni
hadi samaki walio na mimba Ziwa Victoria. Lakini ameshindwa kutoa
takwimu za wanafunzi wanaokwenda shuleni bila viatu wala ‘yebo yebo’.
"Wakati umefika sasa wananchi wa Chato kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu 2015, pigeni kura za
hasira baina ya CCM na huyu Magufuli, kisha kuwachagua viongozi wa
CHADEMA kwa maendeleo yenu," alisema Lwakatare.
|
Ulinzi uliimarishwa eneo la tukio nayo amani ikatawala. |
Kuhusu bei ya pamba,
Lwakatare ambaye amewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia
Chama cha Wananchi (CUF), kabla hajahamia CHADEMA, alisema: "Serikali
ya CCM pamoja na Magufuli imeshindwa kuwasaidia wakulima wa zao hili la
pamba."
|
Dk. Lukanima na wenzie wakitoka kwenye mkutano. |
Kwa upande wake, Dk.
Lukanima aliituhumu CCM na serikali kwa kukosa mwelekeo wa kuwatumikia
na kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
"CCM imekosa mwelekeo. Mimi na usomi wangu huu siwezi kuendelea
kuwa ndani ya CCM ambayo naiona haina faida kabisa kwa Watanzania
wenzangu. Hivi niwaulize ni yupi mwenye unafuu aliyeshika chuma cha
moto na aliyeshika ubao?
"Jibu ni aliyeshika ubao...kwa hiyo njooni tujiunge na CHADEMA
kwa ajili ya ukombozi wa nchi hii. Mfano, hapa Chato hakuna fursa za
kiuchumi, mashirika yamekufa, huduma za kijamii mbovu, na
anayeng’ang’ania CCM ni sawa na usaliti mkubwa wa maendeleo ya taifa
hili," alisema Dk. Lukanima.
Aliwaomba wananchi wa Chato, mkoa na taifa kwa ujumla
kukiunga mkono Chama hicho cha CHADEMA, ili kujikomboa na adha
mbalimbali zinazolikabili taifa na wananchi wake, na kwamba
kilichomsukuma kuhamia chama hicho cha upinzani ni kwenda kuongeza
nguvu katika vuguvugu la mabadiliko.Inatoka kwa mdau.
Comments