JOHANNESBURG, Afrika Kusini
BAO lililofungwa na mshambuliaji Bebe dakika za majeruhi juzi liliiokoa Manchester United ya England isiadhirike baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Ajax Cape Town ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo ilikuwa ya kujipima nguvu kwa Manchester United katika ziara yake ya mechi za kirafiki nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno aliisawazishia Manchester United dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kuunganisha wavuni krosi kutoka pembeni ya uwanja.
Bebe aliingia uwanjani kipindi cha pili sambamba na Dimitir Berbatov, ambaye alishangiliwa kwa mayowe mengi na mashabiki wapatao 54 waliofurika uwanjani.
Ajax ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 86 lililopachikwa wavuni na mshambuliaji wake, Alcardo van Graan.
Katika mechi hiyo, mshambuliaji wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa aliichezea Manchester United mechi yake ya kwanza na nusura afunge bao katika kipindi cha pili.
Sare hiyo iliifanya Manchester United kutopoteza mechi tangu ilipowasili Afrika Kusini. Katika mechi ya kwanza, Manchester United iliichapa Ama Zulu bao 1-0.
Manchester United ilitarajiwa kuondoka jana kwenda China, ambako keshokutwa itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Shanghai Shenhua.

Comments