Mechi
hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Yanga ikiwa chini ya kocha wake mpya, Tom
Saintfiet kutoka Ubelgiji tangu alipoanza kuinoa wiki iliyopita.
Bao
la kwanza la Yanga lilipachikwa wavuni na beki Nadir Haroub 'Cannavaro'
dakika ya 18 kwa shuti baada ya mabeki wa JKT Ruvu kuzembea kuokoa
mpira wa kona.
Hamisi Kiiza aliihakikishia Yanga ushindi
dakika ya 72 baada ya kuifungia bao la pili, kufuatia pande safi
alilomegewa na kiungo Haruna Niyonzima.
Katika mechi
hiyo, beki Kelvin Yondan aling'ara kutokana na kucheza kwa uelewano
mkubwa na Cannavaro, wakisaidiana na kiungo mkabaji, Athumani Iddi
'Chuji'.
Comments