MKURUGENZI
wa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT), ambaye pia ni Mbunge wa Mbinga
Magharibi, John Komba amerejea nchini kutoka India, ambako alikwenda
kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya kumtibu ugonjwa wa nyonga uliokuwa
ukimsumbua upande wa mguu wake wa kulia.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, nyumbani kwake Mbezi kwa Komba, mjini Dar
es Salaam, Komba alisema alirejea nchini juzi baada ya kupatiwa
matibabu hayo kwenye hospitali ya Appolo iliyopo Hydrabad nchini India
tangu mwanzoni mwa wezi huu.
Komba alisema, aliondoka
nchini Julai 2, 2012 baada ya kupelekwa na serikali kwa maelekezo ya
Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge Anna Makinda na Katibu wa Bunge
John Kashilila na kwamba alikwenda baada ya kukosa matibabu hapa nchini
kwa sababu ya mgomo wa madaktari.
Comments