Uswahiba kati ya wasanii wawili wa Bongo Flava nchini,
Afande Sele na 20 Percent umeingia dosari baada ya kutupiana maneno kila mmoja
kwa nyakati tofauti kwenye vyombo vya habari.
Maneno hayo yalianza wiki iliyopita baada ya Afande Sele
kuzungumza na Clouds FM na kudai kusikitishwa na kitendo cha swahiba wake 20
Percent cha kugoma kutumbuiza kwenye tuzo za muziki za Zanzibar wakati alikuwa
amelipwa pesa zote.
Kufuatia mgomo huo, waandaaji walimpeleka lock-up msanii
huyo na kubaki na laptop yake mpaka pale atakapowarudishia waandaji hao
shilingi milioni moja waliyompa kwaajili ya kuperform kwenye tuzo hizo.
Hatimaye jana 20 Percent alizungumza na kituo hicho cha radio
kuhusiana na tukio lenyewe na kusema kuwa Afande Sele amechanganyikiwa na
anasumbuliwa na njaa ndio maana anamlaumu.
Akiongea kwa jaziba, 20 Percent amesema Afande Sele ni
kama ‘mtoto’ na alimshangaa kufahamu kuwa alifika Zanzibar saa sita usiku bila
kuwa sehemu ya kulala kutokana na waandaaji hao kuwa wababaishaji.
Leo (July 14) Afande Sele ametoa maelezo marefu
kuhusiana na sakata hilo kupitia Facebook. Hivi ndivyo alivyoandika:
“Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki
wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twenty
Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi
makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo
yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty
alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na
kumsihi sana ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari
mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi
sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na
kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo
Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM
ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna
yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty
Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili
Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa
na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae
kabla siku za nyuma "MBELE YAKO NYUMA YANGU" .. Kuna mstari Nilisema
" ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugumu, bado unatakiwa uwe
na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu".
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka
enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha'Kingdom, ambao wengine hawafanyi
sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na
kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mmefadhaika kwa hilo.
Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu
lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)
Comments