NA THOBIAS MWANAKATWE
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ameung’ang’ania urais kwa kusema kama urais upo utakuja tu na kwamba hana mashaka na uwezo, uadilifu, uzalendo wake pamoja na kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, ametoa kauli hiyo siku chache, baada gazeti moja (siyo NIPASHE) kuandika kuwa wabunge wawili wa Chadema wamemsafishia njia ya kugombea kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Hata hivyo, juzi ikiwa ni siku moja baada ya kuchapishwa kwa habari hiyo, wabunge hao ambao ni Joshua Nassari (Arumeru Mashariki na Halima Mdee (Kawe) walitoa taarifa katika vyombo vya habari za kutoa kauli za kukanusha na kujiweka mbali na mpango wa kumpigia debe Zitto.
Zitto alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akichangia makadiro ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2012/13.
“Ndugu zangu wasanii, najua kuwa suala la tamasha la Kigoma limeleta maneno maneno kidogo ya kisiasa, lakini hayo ni maneno yatapita kwa sababu kama urais upo utakuja tu, kama haupo hautakuja, hata mtu afanye nini,” alisema na kuongeza:
“Muhimu ni kuhakikisha kuwa tunafanya kazi ya ziada kuitetea nchi yetu na jambo moja tu ambalo sina mashaka nalo hata kidogo ni uwezo, uadilifu, uzalendo wa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi yetu. Hili sina mashaka nalo hata kidogo na kama nina mashaka labda mambo mengine, lakini kwa hili sina mashaka hata kidogo Mheshimiwa Mwenyekiti.”

Comments