Mabingwa
watetezi wa michuano ya soka ya Kombe la Kagame, Yanga juzi wamefufua
matumaini ya kufuzu kucheza robo fainali baada ya kuibugiza Wau Salaam
kutoka Sudan ya Kusini mabao 7-1 katika mechi ya kundi B iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo
ilihudhuriwa na mashabiki wengi wa timu hiyo, wakiongozwa na Mwenyekiti
mpya wa Yanga, Yussuf Manji aliyefuatana na viongozi wenzake wapya. Inatoka kwa mdau.
Comments