Ngasa akiondoka kwenye jukwaa la mashabiki wa Yanga baada ya kuzawadiwa jezi
Mshambuliaji Mrisho Ngasa juzi alifanya vitendo vya ajabu wakati timu
yake ya Azam ilipokuwa ikimenyana na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame.
Katika
mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Ngasa
aliingia uwanjani kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kipre Tchetche.
Kituko
chake cha kwanza ni kwenda kushangilia bao la pili aliloifungua Azam
katika mechi hiyo kwenye jukwaa wanalokaa mashabiki wa Yanga.
Muda
wote wa pambano hilo, mashabiki hao walikuwa wakiizomea Azam, lakini
baada ya mchezaji huyo kufunga bao na kuwafuata, walianza kumshangilia
kwa mayowe mengi.
Comments