Mkurugenzi
wa Global Publishers, Eric Shigongo(kulia) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) juu ya sakata lake na Chameleone. Kushoto ni
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
MD
wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, mapema juzi ameongea na media
kuhusu madai ya Jose Chameleone kudai paspoti yake, ambaye
alikwenda Ubalozi wa Tanzania nchini kwake Uganda kushinikiza
kurejeshewa paspoti yake.
Eric alifunguka kwa kusema
kuwa, kampuni yake na msanii huyo waliingia makubaliano ya kufanya shoo
kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, liliofanyika Uwanja wa Taifa Julai
7 mwaka huu, ambapo katika mazungumzo ya awali, msanii huyo aliomba
kulipwa dola 5000 na kulipiwa tiketi 2 za ndege ili kuhudhuria tamasha
hilo, masharti ambayo yalikubaliwa.
Mazungumzo hayo
ya awali yalifanyika kati ya Global Publishers na agenti wa Chameleone
ajuliikanae kwa jina la George. Kabla ya kutuma fedha hizo, kampuni yake
ilihitaji kujiridhisha kama ajenti huyo alikuwa kweli anawasilina na
kukubaliana na Chameleone kuhusu shoo ya Dar, ili kuepuka utapeli.
“Tulipokubaliana
nae kupitia ajenti wake, tuliamua kwenda mbele zaidi ili kujiridhisha,
ambapo tuliwasiliana na mwanamuziki Kidumu ambaye anamfahamu huyo George
na kwenda mpaka Kampala kukutana ana kwa ana na wahusika, kwa niaba
yetu”, alisema Shigongo.
Akielezea zaidi, Shigongo
alisema kuwa Kidumu alikwenda Kampala na kukutana na George pamoja na
Jose Chameleone, ambaye alikubali kuja kufanya shoo na kumruhusu Kidumu
kusainishana mkataba na ajenti wake na kumpatia hizo fedha.
“Chameleone
alitoa ruhusa kwa ajenti wake kusaini mkataba na kupokea advance ya
dola 3,500 kwa niaba yake kwa madai kuwa yeye asingeweza kusubiri malipo
wakati huo kwa sababu alikuwa anawahi sehemu nyingine.
“Baadae
Jose alikuja kugeuka na kudai hakupewa hizo pesa na ajenti wake, kitu
ambacho kilonekana kama mchezo wa kitapeli kati ya Chameleone na ajenti
wake kwetu sisi.
“Kwa kuwa ujio wake Tanzania ulikuwa
umeshatangazwa sana, uongozi wa Global Publishers, ulilazimika kufanya
mazungumzo mengine na Chameleone na kumuomba sana kuja nchini kufanya
shoo, ambapo this time akakubali kwa masharti ya kulipwa dola 8000 na
tiketi nne za ndege.
“Ndugu zangu, sikua na jinsi,
nililazimika kumkubalia na kumlipa dola 8000, kwa sababu tayari tamasha
lilikuwa limeshatangazwa sana, billboards zimewekwa barabarani na
promosheni kubwa ilikuwa inafanyika,” alisema Shigongo kwa uchungu.
Hivyo
mara baada ya kukubaliana, safari hii akalazimika kumtuma meneja wake
kwenda mpaka Kampala na kukutana na Chameleone ana kwa ana na kumpatia
dola 8000 na kusaini mkataba mwingine wa pili.
“Ni
dhahairi kabisa alichokifanya Chameleone kilikuwa ni utapeli kwa
kushirikiana na ajenti wake, kwa sababu tunamuamini Kidumu, ambaye
tumeshafanya naye kazi mara kadhaa kwa uaminifu mkubwa. Pia ni
Chameleone ndiye aliyemuidhinisha ajenti wake kuchukua pesa hizo, hivyo
ulikuwa ni mchezo wa pamoja, na hiyo ni tabia ya Chameleone, kwani
ameshawafanyia mapromota wengi kiasi kwamba hivi sasa hakanyagi nchini
Kenya.
“Dola 3,500 siyo fedha nyingi, ningeweza
kuzisamehe, lakini nimeamua kuzidai kwa manufaa ya watu wengine.
Watanzania tusikubali kufanywa wajinga kwa sababu ya upole wetu,
tutaendelea kudhauriwa na kufanywa wajinga mpaka lini,” alihoji
Shigongo.
Mwisho Shigongo alitoa wito kwa Watanzania
kuungana katika suala hili, kwani Chameleone ameonyesha dharau kubwa kwa
Watanzania kwa kumfuata balozi wetu nchini Uganda na kuondoka ofisini
kwake huku akisonya na kubamiza mlango, akiendelea kuonyesha dharau kwa
Watanzania wote wapatao miloni 40!
Comments