Pichani kati ni Mwanamuziki mahiri Josee Mara akifafanua kuhusiana na
mikakati yao waliyonayo kwa sasa mara baada ya mwanamuziki mwenzao
mmoja,Kalala Jr kutimka na kuwaacha wakiwa wawili badala ya watatu.
Josee Mara amesema wao wako fiti na hakuna kilichoharibika,kwani kuna
wanamuziki wengine kadhaa ambao ni wazuri na watafanya nao kazi kama
ilivyokuwa kwa Kalala Jr.
"Na sasa hivi nakuhakikishia Da'Suzzy tutapiga
kazi ile mbaya, kwa sababu hao vijana tunaowaongeza ni wanamuziki
wazuri na tunawahamu toka kitambo, kwa hivyo naamini mambo yatakuwa
sawa na washabiki wetu wasivunjike moyo,waendelee kutuunga mkono
tu,sisi ni wapambanaji kwa hiyo ni lazima tupambane"amesema Josee Mara.
Aidha Khalid Chokoraa ameongeza kuwa katika kuonesha bado wako fiti
wamekwisharekodi singo yao moja iitwayo ONA NAONEWA, ambayo
wataitambulisha hivi karibuni kwa mashabiki wa muziki wa dansi

Comments